Pato la taifa au jumla ya pato la taifa (kifupi: JPT) ni kipimo cha thamani ya sokoni ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa ndani ya nchi katika muda fulani.[1]
JPT hutumiwa kwa kawaida na serikali ya nchi ili kupima afya ya uchumi wake. Kipimo hicho mara nyingi hurekebishwa kabla ya kufikiriwa kuwa kiashiria cha kuaminika.[2]