Ramani

Ramani ya dunia ya mwaka 1662
Ramani yaonyesha kilele cha mlima Kilimanjaro na mistari ya kimo
Ramani ya muundo wa usafiri wa reli ndani ya mji wa London, Uingereza

Ramani ni picha - kwa kawaida mchoro - ya dunia au sehemu au sifa zake.

Ni tofauti na picha iliyopigwa kwa kamera kutoka ndege au chombo cha angani kwa sababu mchora ramani anachagua anachotaka kuonyesha na kuzipa uzito sifa anazotaka kuziwekea mkazo.

Kuna aina nyingi za ramani:

Kila mchoraramani anahitaji kuchagua jinsi ya kuonyesha mambo yake. Kwa ramani za kijiografia tatizo hutokana na umbo la dunia ambalo ni tufe wakati ramani kwa kawaida ni karatasi bapa.


Developed by StudentB