Roho

Roho ni umbile la pekee lisiloonekana ambalo linasadikiwa kuwemo pamoja na mwili katika binadamu na kuunda hasa malaika (ambao kati yao wale wabaya wanaitwa mashetani).

Katika lugha mbalimbali umbile hilo linafananishwa na upepo au pumzi.

Mungu mwenyewe anasadikiwa kuwa roho bora. Kwa namna ya pekee Ukristo unasadiki moja ya nafsi za Kimungu ndani ya Utatu inayoitwa Roho Mtakatifu.

Pengine roho inafikiriwa kueleza tofauti kubwa mno ambayo inajitokeza kati ya binadamu na sokwe na wanyama wengine wote upande wa akili na utendaji, na ambayo haielezwi vya kutosha na tofauti katika DNA zao.

Inasadikiwa kuwa roho ndiyo sehemu bora zaidi ya mwanadamu na husadikiwa kuwa haifi bali hudumu milele. Roho humuunganisha mtu na ulimwengu wa kiroho ambao aghalabu huwa ni ulimwengu usioonekana na macho ya kawaida, yaani ya mwili.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Developed by StudentB