Shule ya Antiokia ilikuwa kimojawapo kati ya vituo vikuu viwili vya teolojia na ufafanuzi wa Biblia ya Kikristo wakati wa Mababu wa Kanisa; kingine kilikuwa Shule ya Aleksandria. Majina ya vituo vyote viwili yalitokana na majiji vilipostawi katika Ukristo.
Wakati wanateolojia wa Aleksandria (Misri) walipenda zaidi kufafanua Biblia kiroho, wale wa Antiokia ya Siria (leo nchini Uturuki) walifuata zaidi maneno yenyewe. Matokeo ya tofauti hizo yalijitokeza katika teolojia kuhusu fumbo la Yesu Kristo yakasababisha mafarakano makubwa ya karne ya 5.[1][2]
Historia ya shule ya Antiokia inaweza kugawiwa katika vipindi vitatu: