Tamthilia

Ukumbi wa maonyesho Colon.
Mchoro unaonyesha namna watu wanavyocheza tamthilia.

Tamthilia (pia: Tamthiliya au Tamthilia-Mchezo, kutoka neno la Kiarabu تمثیل ) ni moja kati ya sehemu za utunzi wa hadithi au fasihi simulizi (ngano au hadithi) ambayo mara nyingi tunaona katika kumbi za maonyesho au kupitia televisheni, au tunasikia kupitia redio.

Tamthilia au mchezo mara nyingi huwa mazungumzo baina ya watu ya watu wawili au zaidi, na kwa kawaida huwa mchezo hatuutazami katika televisheni tu, bali hata kuna watu wengine hufuatilia kwa kupitia maandiko yenye tamthiliya hizo na kuzielewa vyema.

Watu tunaowaona wanafanya tamthilia ni waigizaji; katika ukumbi wa maonyesho husimama juu ya jukwaa na kuanza kutoa burudani yao huku watu wakiwaangalia (watazamaji) wanaweza wakawaona vyema kabisa.

Mwongozaji anawasaidia waigizaji kufanya kazi zao vyema na kutoa muongozo Kwa waigizaji, au anawaeleza namna ya mchezo jinsi unavyotakiwa kuchezwa.


Developed by StudentB