Trekta

Trekta ya Volvo ya mwaka 1956
Trekta ya mvuke mwaka 1904
Trekta ya kisasa ya kuendeshwa kwa magurudumu yote manne

Trekta (kutoka lat./ing. tractor "mvutaji") ni gari maalumu linalotumiwa hasa katika kilimo.[1]

Kwa kawaida huwa na kiti kimoja cha dereva pekee na kusudi lake si usafiri wa watu lakini kuvuta (au kuendesha) mitambo mbalimbali au trela yenye mzigo.

Nje ya kilimo hutumiwa katika uchumi wa msituni, kwenye kazi za ujenzi na pia kwenye uwanja wa ndege.

  1. Colour Oxford English Dictionary (tol. la Second). Oxford University Press. 2002. uk. 747. ISBN 0198605692.

Developed by StudentB