Uchafuzi wa bahari ni hali inayotokana na shughuli mbalimbali zinazohatarisha mazingira ya bahari.
Shughuli hizi mara nyingi hutokana na binadamu mwenyewe, katika hali ya kujitafutia riziki za kila siku, hususani katika kipindi hiki cha ukuaji wa teknolojia za viwanda, na mara nyingi huwa ni za uvuvi baharini pamoja na zile ambazo hufanyika karibu au pembezoni mwa bahari husika.
Bahari za dunia kwa karne nyingi zimeonekana kuwa sehemu mahususi za kutupia taka. Hivyo sasa imepelekea kwa wingi kiasi kikubwa cha uchafu kimezidi kuwa kingi sana, mpaka hupelekea athari katika bahari kuu kwa viumbe wanaoishi ndani yake.
Uchafuzi huu wa bahari kwa kiasi kikubwa huonekana katika fukwe za bahari kuu ambazo hupokea kila aina ya uchafu unaotokana na shughuli za binadamu.