Uchafuzi wa hewa ni uingizaji wa mata yenye madhara kwa uhai katika hewa inayozingira dunia, hata kusababisha maradhi, vifo na uharibifu wa aina mbalimbali kwa binadamu na viumbe hai vingine, vikiwa pamoja na mazao.[1]
Vyanzo vyake hujumuishwa na vyombo vya moto, viwanda vya kuvuna umeme, viwanda vingine na shughuli za kila siku za nyumbani.
Kwa namna ya pekee uchafuzi huo umefanyika na kuathiri Ulaya, Amerika na maeneo mengi ya Asia.
Uchafuzi wa hewa ni mbaya zaidi mijini ambako umesababisha ongezeko kubwa la madhara ya kupumua kwa wakazi wengi sana.
Kadiri ya ripoti ya mwaka 2014 ya WHO, mwaka 2012 uchafuzi ulisababisha vifo vya watu milioni 7 duniani kote.[2]
{{cite web}}
: Unknown parameter |deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)