Uislamu kwa nchi |
Uislamu nchini Kenya unakadiriwa kufikia asilimia 11.1 ya wakazi wote wa Kenya[1], au makadirio ya milioni 4.3 ya watu.
Sehemu kubwa ya pwani ya Kenya imejawa na wakazi wengi wa Kiislamu, lakini Nairobi pia ina misikiti kadhaa na Waislamu kadhaa maarufu.
Sehemu kubwa ya Waislamu wa Kenya ni wafuasi wa dhehebu la Sunni wanaofuata mafundisho ya Shafi. Vilevile kuna kiasi kadhaa cha Waislamu wanaoafuata dhehebu la Shia na Ahmadiyya.[2] Katika sehemu kubwa, Shia ni Waismailia waliotokana au wenye athira kutokana na wafanyabiashara wa majini/bahari kutoka Mashariki ya Kati na India. Hao Washia ni pamoja na Dawoodi Bohra, ambao wanakadiriwa kuwa kati ya 6,000-8,000 nchini humo.[3]
{{cite web}}
: Unknown parameter |=
ignored (help)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)