Unguja

Ramani ya Unguja

Unguja ni kisiwa kikubwa katika Bahari Hindi mkabala wa mwambao wa Afrika ya Mashariki karibu na Dar es Salaam.

Unguja ndicho kisiwa kikuu cha funguvisiwa la Zanzibar ambavyo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Unguja ina eneo la takriban km² 1.658 ikiwa na wakazi 869,721 (2012).

Mji mkuu ni Jiji la Zanzibar kwenye pwani ya magharibi mkabala wa bara.

Kisiwani Unguja kuna mitatu kati ya mikoa 31 ya Tanzania ambayo ni Unguja Kaskazini, Unguja Kusini na Unguja Mjini Magharibi.


Developed by StudentB