Upimaji dunia au Jiodesia (kutoka Kigiriki: γεωδαισία, geodaisia, yaani mgawanyo wa dunia; pia: Jiodisi kupitia Kiingereza "Geodesy") ni sayansi ya dunia inayohusika na upimaji na uelewaji wa umbo lake, mwelekeo wake angani, na uvutano wake.
Utafiti wake unaenea katika mabadiliko ya tabia hizo za dunia na katika zile za sayari nyingine.