Waraka wa kwanza wa Yohane

Agano Jipya

Waraka wa kwanza wa Yohane ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Barua tatu za Yohane ziliandikwa kati ya mwaka 90 na 100 B.K., wakati ambapo jumuia za wafuasi wa Mtume Yohane zilianza kusambaratika.

Mafundisho na lugha vinalingana na vile vya Injili ya nne (Injili ya Yohane).

Barua ya tatu na ya pili hazina mafundisho muhimu, tofauti na ile ya kwanza inayodai imani sahihi na maisha matakatifu ili mtu astahili kuitwa Mkristo kweli.

Inakaza umwilisho wa Mwana wa Mungu na haja ya kuishi kwa uadilifu, na hasa kwa upendo (1Yoh 1:1-4; 2:3-11; 3:11-4:21; 2Yoh 7-13).


Developed by StudentB