Jiji la Washington | |||
| |||
Mahali pa mji wa Washington katika Marekani |
|||
Majiranukta: 38°54′36″N 77°0′36″W / 38.91000°N 77.01000°W | |||
Nchi | Marekani | ||
---|---|---|---|
Tovuti: http://www.dc.gov/ |
Washington D.C. ni mji mkuu wa Marekani mwenye wakazi 553,523. Kifupi "D.C." baada ya jina chamaanisha "District of Colombia" ambayo ni mkoa wa shirikisho yaani eneo lililotengwa moja kwa moja kwa vyombo vya shirikisho la Marekani kwa sababu maeneo mengine ya Marekani yako chini ya majimbo mbalimbali yanayojitawala.
Jina la mji mkuu limechaguliwa kwa heshima ya kiongozi wa uhuru na rais wa kwanza George Washington. Jina la "District of Colombia" likachaguliwa kwa heshima ya Kristoforo Kolumbus mpelelezi wa Amerika.
Mji wa Washington uko kando la mto Potomac kati ya majimbo ya Maryland na Virginia. Uko karibu na pwani la mashariki la Marekani. Hori ya Chesapeake ya Atlantiki iko 35 km kutoka mji. Anwani ya kijiografia ni 38°53'42"N na 77°2'12"W.
Washington D.C. ni tofauti na jimbo la Washington lililopo upande wa magahribi wa Marekani.
Hapa ni makao rasmi ya Bunge la Marekani, ya Rais pamoja na serikali yake na makao ya mahakama kuu. Kuna pia majengo ya kihistoria hata kama Marekani haina historia ndefu pamoja na makumbusho mazuri.