Yerevan (pia: Erevan, Erivan; kwa Kiarmenia: Երեւան au Երևան) ni mji mkuu na pia mji mkubwa wa Armenia.
Idadi ya wakazi ni juu ya milioni moja (mwaka 2004).
Iko kando ya mto Hrazdan na kutazama mlima Ararat ambao ni mlima mtakatifu wa Waarmenia.
Mji ni wa kale: ulianzishwa kama boma la Erevuni katika milki ya Urartu mnamo 782 KK.