| |||||
Kaulimbiu ya taifa: {{{national_motto}}} | |||||
Wimbo wa taifa: عاش المليك ' ash al-malik "Heri kwa mfalme" | |||||
Mji mkuu | Amman | ||||
Mji mkubwa nchini | Amman | ||||
Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
Serikali | Ufalme wa Kikatiba Abdullah II Bisher Al-Khasawneh | ||||
Uhuru Tarehe |
25 Mei 1946 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
89,342 km² (ya 112) 0.8 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2019 kadirio - 2015 sensa - Msongamano wa watu |
10,407,793 (ya 86) 9,531,712 114/km² (ya 70) | ||||
Fedha | Dinar ya Yordani (JOD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UTC+2 (UTC+2) UTC+3 (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | .jo | ||||
Kodi ya simu | +962
|
Yordani (pia: Jordan, Jordani; kwa Kiarabu; الأردنّ "al-urdun") ni ufalme wa Kiarabu katika Mashariki ya Kati.
Jina la nchi limetokana na mto Yordani ambao ni mpaka wake upande wa magharibi na Israel na eneo la Palestina ya leo.
Jina rasmi ni Ufalme wa Kihashemi wa Yordani (kwa Kiarabu: المملكة الأردنية الهاشمية ) kutokana na familia ya kifalme.
Imepakana na Syria, Iraq, Saudi Arabia, Palestina na Israeli.
Ina pwani fupi kwenye Ghuba ya Aqaba ya Bahari ya Shamu.