Zana

Visu ilikuwa moja kati ya zana za kwanza zilizotengezwa na wanadamu.

Zana ni kifaa chochote ambacho hutumiwa na binadamu ili kuweza kumrahisishia kazi zake za kila siku na kuleta ufanisi katika matokeo ya kazi anayoifanya pamoja na kuhifadhi muda.

Mifano ya zana ni jembe la mkono, toroli, mashine ya kufyatua tofali, kisu, panga na nyingine nyingi ambazo hurahisisha kazi.

Zana zina faida mbalimbali ambazo ni:

  1. Husababisha ufanisi wa kazi
  2. Huokoa muda kwani kazi humalizika baada ya muda mfupi
  3. Huongeza uzalishaji
  4. Husaidia katika kuboresha bidhaa

Kwa ujumla zana ni chombo muhimu sana katika maisha ya kila siku ya binadamu ili kuleta maendeleo katika jamii.


Developed by StudentB