Valensi (kwa Kiingereza: valency au valence) ni istilahi ya kemia inayotaja nguvu ya atomu ya kuunda muungo kemia na atomu nyingine. Inataja idadi ya miungo inayoweza kuundwa baina ya atomu ya elementi fulani pamoja na hidrojeni (iliyo elementi sahili zaidi).